LENZI Podcast with Michael Kamukulu

Michael Kamukulu

Jifunze kupitia mijadala na maelezo yanayohusu mada mbalimbali ili upate ufahamu juu mienendo ya sasa katika nyanja na tasnia tofauti. Pata uchambuzi wa takwimu rasmi katika kuleta uhalisia wa mada tunazozijadili. Uwe ni mmiliki wa biashara unayetaka kuboresha biashara yako ama kufungua mradi mpya, au mtu binafsi unayetaka kuongeza ufanisi wako, podcast yetu ina kitu kwa ajili yako. SIKILIZA ILI UWEZE KUJIFUNZA read less
EducationEducation

Episodes

S1E21 Digital Detox: Jinsi nilivyojiondoa kwenye addiction ya SIMU na Mitandao | Michael Kamukulu LENZI
Oct 28 2023
S1E21 Digital Detox: Jinsi nilivyojiondoa kwenye addiction ya SIMU na Mitandao | Michael Kamukulu LENZI
DIGITAL DETOX Watumiaji wengi hawazifahamu athari zinazotokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii, simu, TV pamoja na aina nyingine ya vifaa vinavyotumia screen. Athari hizi zina madhara makubwa sana ikiwemno kusababisha changamoto za afya ya akili. Athari nyingine ni kama matumizi mabaya ya muda, kupunguza ufanisi kwenye uzalishaji, kuvunjika kwa mahusiano pamoja na madhara mengine mengi. Mawasiliano ni kitu cha kuhimu lakini ni muhimu kufuatilia miendendo ya matumizi ya simu za mkononi na mitandao ili kuepuka madhara na athari mbaya. Punguza matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii na simu za mkononi ili ulinde maisha na afya yako. Kabla ya kukabiliana na athari hizi, ni muhimu sana mtu akafahamu kama tayari anapitia changamoto hizi au la. Kuna njia nyingi za kutammbua kama umeathiriwa na matumizi makubwa ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii. Njia rahisi ni kuangalia kama una mojawapo ya dalili zifuatazo: 1. Kutopendelea kuzungumza na watu, na badala yake kukaa na simu za mkononi au mitandao ya kijamii 2. Kuwa na hali ya wasiswasi uliopitiliza mara kwa mara (Anxiety) 3. Kukosa usingizi (kushindwa kulala vizuri) 4. Kushindwa kutuliza akili (failure to focus) Zipo njia nyingi za kuondokana na madhara ya matumizi yaliyopitiliza ya mitandao ya kijamii na simu za mkononi pamoja na TV.; kati ya hizi ni hizi hapa tano (5): 1. KUTENGA MUDA wa kukaa bila simu/mitandao 2. Kudhibiti APPS 3. Kudhibiti MUDA wa matumizi 4. Kudhibiti MAENEO ya matumizi 5. Balance: Maisha BINAFSI na Maisha ya KAZI Ungana na Michael Kamukulu uweze kujifunza zaidi kupitia LENZI  @lenzipodcast  Chapters 00:00 Madhara: matumizi yaliyopitiliza ya simu na mitandao 01:33 Digital Detox 02:36 1. KUTENGA MUDA wa kukaa bila simu/mitandao 04:26 2. Kudhibiti APPS 06:43 3. Kudhibiti MUDA wa matumizi 08:13 4. Kudhibiti MAENEO ya matumizi 08:39 5. Balance: Maisha BINAFSI na Maisha ya KAZI Jifunze zaidi na Michael Kamukulu kupitia LENZI @lenzipodcast
S1E20 Matumizi ya SIMU: Fahamu athari za matumizi yaliyopitiliza ya simu | LENZI | Michael Kamukulu
Oct 21 2023
S1E20 Matumizi ya SIMU: Fahamu athari za matumizi yaliyopitiliza ya simu | LENZI | Michael Kamukulu
Watumiaji wengi hawazifahamu athari zinazotokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii, simu, TV pamoja na aina nyingine ya vifaa vinavyotumia screen. Athari hizi zina madhara makubwa sana ikiwemno kusababisha changamoto za afya ya akili. Athari nyingine ni kama matumizi mabaya ya muda, kupunguza ufanisi kwenye uzalishaji, kuvunjika kwa mahusiano pamoja na madhara mengine mengi. Mawasiliano ni kitu cha kuhimu lakini ni muhimu kufuatilia miendendo ya matumizi ya simu za mkononi na mitandao ili kuepuka madhara na athari mbaya. Punguza matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii na simu za mkononi ili ulinde maisha na afya yako. Kabla ya kukabiliana na athari hizi, ni muhimu sana mtu akafahamu kama tayari anapitia changamoto hizi au la. Kuna njia nyingi za kutammbua kama umeathiriwa na matumizi makubwa ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii. Njia rahisi ni kuangalia kama una mojawapo ya dalili zifuatazo: 1. Kutopendelea kuzungumza na watu, na badala yake kukaa na simu za mkononi au mitandao ya kijamii 2. Kuwa na hali ya wasiswasi uliopitiliza mara kwa mara (Anxiety) 3. Kukosa usingizi (kushindwa kulala vizuri) 4. Kushindwa kutuliza akili (failure to focus) Zipo njia nyingi za kuondokana na madhara ya matumizi yaliyopitiliza ya mitandao ya kijamii na simu za mkononi pamoja na TV. Fuatilia zaidi uweze kujifunza na Michael Kamukulu kupitia LENZI  @lenzipodcast #mitandaoyakijamii #digitaldetox #mitandao #socialmedia #overused #lenzi #afyayaakili #afyayako #simuyako * * * Timestamps 00:00 Ukweli kuhusu matumizi ya simu na mitandao 01:55 1. Kupendelea kutozungumza na watu 03:49 2. Wasiswasi uliozidi (Anxiety) 04:59 3. Kukosa Usingizi (kushindwa kulala) 05:32 4. Kushindwa kutuliza akili (failure to focus) 06:54 Jinsi ya kujiondoa kwenye madhara ya matumizi makubwa ya simu na mitandao ya kijamii
S1E16 Harufu Ya Chakula Haitibu Njaa: Furaha inayotegemea kuwaridhisha watu wengine bila faida binafsi, ni UTUMWA
Sep 23 2023
S1E16 Harufu Ya Chakula Haitibu Njaa: Furaha inayotegemea kuwaridhisha watu wengine bila faida binafsi, ni UTUMWA
Njaa hutibiwa na chakula, wala harufu nzuri na hata sio lazima chakula kiwe kitamu sana. Haijalishi kama kinaliwa jioni, mchana, asubuhi wala usiku. Harufu ni hisia inayokuvutia kuelekea kwenye chakula, lakini usipokula hicho chakula, njaa haitaondoka. Hii inatokea sana kwenye maisha yetu ya kila siku katika kutafuta mafanikio ya career, mahusiano, nk. Tunahitaji maarifa sahihi ili kufanya maamuzi sahihi yatakayotupa kufanikiwa kwenye kazi, kukuza faida kwenye biashara, kuongeza wigo kama viongozi / kiongozi, kuboresha mahusiano ndani na nje ya ndoa pamoja na mambo mengine mengi. Mojawapo ya njia za kuongeza mafanikio yanayotokana na maamuzi yetu ni kujitambua, kuweka malengo na kuwa na uwezo wa kuyapima malengo kwa kipimo sahihi. Zipo siri na kanuni nyingi ambazo zinaweza kumsaidia kila mtu, lakini walio wengi wamechagua hisia kuliko uhalisia. Watu wengi hupima mafanikio ya maamuzi yao katika maisha, biashara, mahusiano hata kazi kwa kuangalia ni kwa kiasi jamii ikiyowazunguka inaridhishwa. Hata kama itahusisha maumivu, hasara au majuto, bado watu walio wengi wako tayari kufanya jambo wasilolitaka ilimradi wengine wawakubali na kuwaheshimu. Si mara zote matokeo yanakuwa chanya, na ndio maana kuna umuhimu wa kuangalia faida zote, binafsi na zile za jumla ili matokeo ya maamuzi yoyote yale yasije yakaishia kuwa majuto, hasira, chuki, aibu ama kukata tamaa. * * * Hadithi/Simulizi Mtoto (yatima) aliomba chakula cha kwake na wadogo zake ili wasife njaa baada ya kukaa siku nyingi bila mlo wowote. Mtu mzima aliyeombwa chakula alimjibu kwa kutoa ushauri, “chukua kitunguu swaumu ukakichome kwenye moto, majirani wakisikia watasema mmepika na kuka chakula kizuri”. Huu ushauri haukulenga kutatua tatizo halisia, ulilenga kuionesha jamii kwamba hakuna tatizo wakati huo huo madhara yakiendelea kutokea kwa watoto. * * * Ongeza uwezo wako katika kufanya maamuzi sahihi kwa kutumia njia bora ambazo hazina madhara. Sikiliza uweze kujifunza zaidi na Michael Kamukulu kupitia LENZI |  @lenzipodcast
S1E10 SIRI 5 za KUKUA, na KUFANIKIWA kwenye KAZI (AJIRA) na maisha
Aug 5 2023
S1E10 SIRI 5 za KUKUA, na KUFANIKIWA kwenye KAZI (AJIRA) na maisha
Elimu rasmi ni muhimu sana katika kufungua milango ya kazi (ajira); lakini vyeti peke yake havitoshi kukupa mafanikio unayotamanni kuyapata kwenye Maisha kwa kupitia kazi/ajira yako. Kuna mbinu na kanuni nyingi ambazo hazifundishwi kwenye mifumo ya elimu rasmi lakini zinapatikana mtaani baada ya kuanza kufanya kazi. Mfanyakazi yeyote asiyejiendeleza (binafsi) kwa kuongeza maarifa yake katika anachokifanya na zaidi ya hichi anachokifanya, uwezekano wake wa kufanikiwa kwenye Maisha ni mdogo. Kupata madaraja ya juu ya ufaulu shuleni au vyuoni sio kigezo cha kupata mafanikio makubwa kwenye Maisha. Ni muhimu pia kujua mafanikio ni kitu gani. Endapo mtu ataweka malengo ya kufanya kitu fulani kwa wakati Fulani na akafanya hivyo, basi amefanikiwa; na kinyume chake. Hivyo basi, mafanikio yanahoitaji kupimwa kwa vigezo vya (1) Malengo na (2) Muda. Malengo yanatakiwa kuwekwa katika vipindi vywa muda mfupi na muda mrefu pia ili kupima maendeleo kwenye vipindi vifupi vifupi na kupima mafanikio ya jumla (muda mrefu) ifikapio mwishi wa safari.   Kutokana na mabadiliko ya maendeleo na teknolijia, baadhi ya kazi zitaendela kupoteza umuhimu wako jambo litakalopelekea kazi hizo kutoweka sokoni taratibu mpaka hapo zitakapokwisha kabisa, kwa sababu hakuna mtu yeyote atakayekuwa akizihitaji. Kwa upande mwingine, KAZI mpya zinazaliwa kila siku na uhitaji wake katika soko ni mkubwa kwa sababu ujuzii na maarifa yanayoamnbatana na kazi hizo ni adimu. Kazi mpya zina nafasi kubwa ya kumpa mtu nafasi ya kupata kipato kizuri, kukua na kuongezeka na hatimaye kufanikiwa kwenye Maisha nje ya kazi.