S1E12 Kwa nini hatuwezi kulipa madeni?? (2/3 ya watanzania hawawezi kumudu gharama za maisha)

LENZI Podcast with Michael Kamukulu

19-08-2023 • 13 mins

Ripoti ya @finscope ya 2023 imeongelea mambo mengi ikiwa ni pamoja na sababu zinazowafanya Watanzania kukopa fedha. Katika kuichambua zaidi hii ripoti na kuunganisha taarifa nyingine (nje ya ripoti) tumegundua kuwa watu wengi wanaamini kwamba kumekuwepo na u]kukosekana kwa uaminifu baina yta watu hususani kwenye masuala ya kifedha ambapo watu walio wengi wanakopa na wanakuwa hawalipi madeni yao. Uaminifu sio sababu PEKEE inayopelekea watu kutolipa madeni yao, kuna sababu nyingine kama vile kutokuwa na ELIMU sahihi kuhusu masuala ya kifedha, ugumu wa maisha (kipato kidogo) - jambo ambalo linasababisha watu kukosa njia ya kuzalisha (kutengengeza) kipato cha kutosha na kmwisho wa siku kuamua kuweka kipaumbele kwenye kuishi (survive) na sio kulipa madeni yao. Lakini kwa upande mwingine, kukopa kumegeuka kuwa mtindo wa maisha kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakichukulia kukopa kama njia rahisi ya kutatua matatizo hata yale ambayo yasingehitaji mkopo endapo wangefikira kwa umakini madhara ambayo yangejitokeza endapo wangechukua mikopo katika hali walizonazo za kiuchumi. Madhara ya mikopo yamekuwa ni makubwa yakijumuisha kuvunjiuka kwa urafiki, familia na hata baadhi ya ndoa. Ungana na Michael Kamukulu ujifunze zaidi kwenye LENZI @lenzipodcast