S1E15 Ishara 5 kwamba unapoteza kuliko unavyopata (unapoteza MUDA, THAMANI, FEDHA kwenye kazi na biashara)

LENZI Podcast with Michael Kamukulu

16-09-2023 • 8 mins

Kama hasara ama gharama ya kupata jambo lolote inakuwa kubwa kuliko faida zinazotokana na jambo hilo, basi hatuna budi kuachana na jambo husika na kutafuta mbadala unataofaa na kutupa manufaa tunayoyahitaji. Kama gharama za matumizi zinazidi kiwango cha mshahara ama faida ya biashara, ni wakati wa kubadilisha kazi au biashara hiyo. Mara nyingine inakuwa vigumu kufahamu kwamba tayari uko kwenye hali ya kupoteza na kuliko kunufaika. Hizi ni ishara 5 kati ya nyingi zinazokufungua macho ili kujua kwamba ni wakati wa kufanya jambo tofauti. 1. Gharama za matumizi ni kubwa kuliko kipato (mshaharara au faida ya biashara) 2. Kutokuona mabadiliko (matokeo) yanayotokana na kazi au biashara 3. Kushindwa kumiliki na kusimamia muda na ratiba binafsi 4. Kushindwa kuishi katika uhalisia wa ndani (failure to be your authentic self) 5. Kushindwa kutumia uwezo binafsi (vipaji na karama) Ungana na Michael Kamukulu ili kujifunza zaidi kupitia LENZI | @lenzipodcast