S1E17 Jinsi ya Kufanya Manunuzi Salama Mtandaoni: Mambo Matano (5) ya Muhimu | LENZI | Michael Kamukulu

LENZI Podcast with Michael Kamukulu

30-09-2023 • 5 mins

Watu walio wengi hawajui jinsi ya kununua bidhaa kwa njia salama kwenye mtandao kama vile Alibaba, Amazon, Kikuu, Ali Express na mitandao mingine ya aina hii. Kabla ya kuagiza bidhaa kwenye mtandao au simu, ni muhimu kuhakikisha kwamba pesa yako iko salama na unanunua kwa wauzaji wanaoaminika. Unaweza kutumia njia kama vile M Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money au nyingine kama vile Sim Banking. Na unaweza pia ukaagiza buidhaa kwa delivery na ukalipia cash baada ya kupokea bidhaa yako. Ni muhimu kujua Mamboi matano (5) muhimu ambayo yatakusaidia kuwa salama wakati wa manunuzi ya mtandaoni: 1. Kuwa na Akaunti Maalum ya Malipo 2. Nunua kwa Wauzaji Wanaoaminika 3. Tunza/Ficha Taarifa Zako zote Muhimu 4. Fanya Mawasiliano ya kina na Muuzaji kabla ya kununua/kulipia 5. Usifanye Manunuzi Makubwa kwa njia ya Mtandao Fuatilia na ujifunze zaidi na Michael Kamukulu kupitia LENZI @lenzipodcast